Facebook Twitter Delicious Stumble Upon
0 comments

Mauaji ya kinyama

Kijana wa miaka saba apatikana ameuawa na sehemu zake za siri kutolewa katika kijiji cha Msambweni Kaunti ya Kwale.
Kulingana na mamake mtoto kijana wake alichukuliwa na rafikiye ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili ya Waa, mwendo wa saa tatu asubuhi lakini hakuonekana tena hadi mwendo wa jioni ambapo juhudi za kumtafuta zilianza ili aweze kufungua (futhuru) na wazaziwe. juhudi hizo zilipogonga mwamba ndipo walichukua fursa ya kupiga ripoti kwa polisi na kijana huyo kutiwa nguvuni na kufichua kwamba alimlawiti kabla ya kumtoa uhaii.
Polisi wameahidi kufanya uchunguzi zaidi.
0 comments
Anyeshewa na mawe kwa tuhuma za ulawiti
Jamaa mmoja aponea chupuchupu kutoka kwa wananchi wenya ghathabu baada ya kufumaniwa akilawiti kakake mdogo.
Askari waliokua wakipiga patroli walimuokoa jamaa huyo  ambaye siku zake za mwisho zilikua zamkodelea macho, na kumfikisha katika kituo cha polisi cha Nyali.Ingawa haijabainika ni kwa kipindi cha mda gani jamaa huyo amekua akitenda kitendo hicho, ripoti za daktari zadhihirisha kwamba ndugu huyo amekua akifanya tukio hilo mara kwa mara kwa nduguye ambaye kwa sasa hana akili timamu.